Klabu ya Simba SC imefanikiwa kuinasa saini ya mlinzi wa kulia Kelvin Kijili kutoka Singida Fountain Gate kwa mkataba wa miaka miwili.
Kijili mwenye umri wa miaka 24 ni kijana mwenye kipaji na kasi na amekuwa akitumika kuanzisha mashambulizi kutokea upande wa kulia.
Akiwa na Singida Fountain Gate msimu uliopita Kijili amesaidia kupatikana kwa mabao manne (assist).
Kijili anatarajiwa kuongeza nguvu kubwa kwenye kikosi cha klabu hio na kutokana na umri alionao ataendelea kuwa msaada kwa timu kwa muda mrefu.
Usajili tunaofanywa kuelekea msimu mpya wa mashindano umezingatia kigezo cha umri kwakuwa malengo ya Simba SC ni kujenga timu imara ya muda mrefu.
Tayari Kijili amejiunga na wenzake kambini nchini Misri kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2024/25.
#KonceptTvUpdates