Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inatekeleza mapendekzo ya tume ya haki jinai kwa kujenga ofisi za kamanda mikoa katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na kuweka vitendea kazi vya kisasa na kuboresha vituo vya polisi.
Dkt Samia ametoa rai hiyo leo Julai 14 wakati akifungua jengo la kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi na kusema kwamba “Ukiangalia jengo hili, hapa tumetimiza mapendekezo yote ya ile tume, kuweka mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa jeshi la polisi,kuweka vitendea kazi, hilo ni pendekezo la tume ya haki jinai” Amesema Dkt Samia.
Mhe Rais ameongeza “ jengo la namna hii tumejenga maeneo mengi Tanzania na yote yana hadhi kama jengo hili,lakini tuna kazi ya kuboresha vituo vya polisi katika maeneo mbalimbali, kazi ambayo imeshaanza”
Aidha Mhe Rais ametoa maagizo ya kuhakikisha jeshi la polisi linafanya kazi kwa kuzingatia utawala bora ili kuleta amani na utulivu ndani ya nchi.