KOcha i Gareth Southgate ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake katika timu ya taifa ya England baada ya kupoteza kwenye michezo miwili mfululizo ya fainali ya EURO 2020 na 2024 dhidi ya Uhispania mjini Berlin nchini Ujerumani.
Southgate mwenye umri wa miaka 53 amesema “Najivunia kuwa Muingereza,ni heshima kubwa kwenye maisha yangu kuichezea England na kuifundisha England lakini kwa sasa ni muda wa mabadiliko na ukurasa mpya ndani ya timu”
Gareth Southgate amedumu ndani ya England kwa miaka 8 huku ameiongoza kwenye michezo 102 na kuifikisha kwenye fainali mbili za EURO pamoja na nusu fainali ya kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.