Rais wa Marekani, Joe Biden ametangaza kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha Urais wa Nchi hiyo ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba huku akisema hivi karibuni atahutubia Taifa hilo na kuweka msimamo wake huo.
Akitangaza uamuzi huo Biden amesema imekuwa heshima kubwa zaidi ya maisha yake kuhudumu kama Rais wa Nchi hiyo lakini ameamua kujiondoa huku akiamini kuwa ni kwa maslahi bora ya chama chake na nchi kusimama huku akiangazia kutimiza majukumu kama Rais kwa kipindi kilichosalia cha muhula wake.
Biden amelazima kuweka barua kwenye mitandao ya kijamii baada ya wiki kadhaa za shinikizo kutoka kwa Wanademokrasia wengi wakitia shaka uwezo wake wa akili katika umri alionao wa miaka 81.