Sakata la Mwanachama wa Klabu ya Yanga, Juma Magoma kulishitaki Baraza la Wadhamini wa klabu hiyo akidai kuwa katiba inayotumika kwa sasa si halali kwani yeye anatambua katiba halali ni ile ya mwaka 1968 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.
Juma Magoma alidai kuwa kina Haji Manara na Ally Kamwe ni mamluki ndani ya Yanga kwani ni mashabiki wa Simba waliotumwa kuja kuivuruga Yanga.
Manara amejibu hoja hiyo; “Magoma ana haki gani ya kuzungumza uhalali wangu Yanga? Anapata wapi? Mimi nimezaliwa Yanga. Tumeshinda ubingwa mara 30, familia ya Manara tumechangia ubingwa mara 15, yani Magoma alete mpasuko Yanga? Nyie mmelogwa mna ukichaa, Magoma yule? Wewe unaijua Yanga au unaisikia? Ana habati kaikuta Yanga hii ina wastaarabu, ingekuwa Yanga ile kwani hata angesema?
“Kwanza alikuwa wapi mbona mimi sijawahi kumuona, mimi nimekuwa nyumba tatu kutoka Yanga yeye alikuwa wapi? Yanga ipi alikuwa anakwenda? Haijui Yanga wala hajawahi kuitumikia Yanga, yeye kazi yake ni migogoro tu, akimaliza wa Manara, kaenda kwa Manji, anahamia wa GSM, anakwenda wa Eng. Hersi. Nimemwambia Hersi kaa kimya wewe ndiye Rais wa wa Klabu hii (Yanga).
“Tunajua nyuma yake kuna nani, wengine wapo ndani ya Yanga, wamevuliwa udhamini, yule hana uwezo wa kulipa kodi ya nyumba anaweza kulipa wakili? Tunamjua yuko mtu ndani ya Yanga ambaye ameondolewa katika udhamini, ninamfuga leo tu mpaka kesho.
“Yule anafanya uchale kama machale wengine, Yanga ni ya kuteteleshwa na magoma? Hivi nyie yanga mnaijua kweli? Mie ni Yanga kuliko yeye, nimezaliwa pale, anauliza mimi nani? Mimi ndiyo mwenye Yanga.
“Magoma Magoma Magoma, mimi mhuni sana naigiza tu ustaarabu, nimezaliwa na kukulia Downtown Kariakoo, sikutoka Mbwinde mimi, chezea wengine mimi ntakuja kukuwamba makofi hadharani. Hizi suti tunazuga tu.
“Ole wako unitaje tena kwa lolote lile, wahangaishe wageni sio mimi niliozaliwa Jangwani, familia yetu imeshinda kila kitu pale Yanga kuliko familia yoyote ile, tuna contribution kubwa sana. Usiniguse na keep distance with Buga, usinilazimishe nitumie maarifa yangu ya Kung fu niliyoyapata Guandong. Ole wako unitaje tena,” amesema Manara.