Wakati Mzee Magoma akizidi kukamata vichwa vya wapenda michezo nchini kutokana na sakata lake na uongozi wa Klabu ya Yanga.
Upande wa pili klabu ya Simba inajiandaa na maandalizi ya Tamasha lake kubwa la “Simba Day” linalotarajiwa kufanyika Agosti 3 mwaka huu katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Sasa katika hali ya kushangaza, Meneja wa Habari na Mawasiliano ya Klabu ya Simba, Ahmed Ally kupitia Ukurasa wake wa Instagram ameandika “Mgeni Rasmi Simba Day ni Mzee Magoma … Ubaya Ubwela”
Haijulikani kama Meneja wa Habari na Mawasiliano huyo anafanya utani ama anamaanisha alichokiandika.