Baada ya maswali mengi kuhusu wapi alipo mchezaji Kibu Dennis, klabu ya Simba Sc imevunja ukimya na kuutaarifu umma kuwa nyota huyo raia wa Tanzania hajaripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2024/2025.
Taarifa ya Wekundu hao wa Msimbazi imebainisha kuwa klabu hiyo ilimuongezea Kibu mkataba wa miaka miwili zaidi utakaoisha, Juni 2026 na kumlipa stahiki zake zote za kimkataba mchezaji huyo ambaye alifunga goli moja tu msimu uliopita amekuwa akitoa sababu kadha wa kadha zinazomfanya kushindwa kuripoti kambini.
Kutokana na utovu huo wa kinidhamu klabu hiyo imesema itamchukulia hatua stahiki za kinidhamu na “umma utapewa taarifa”