Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Theopista Mallya amethibitisha kutokea Kwa vifo vya Wanawake wawili ambapo katika uchunguzi wamebaini Wanawake hao hawakuuawa.
Kamanda Mallya ameyasema hayo Julai 23,2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo amesema baada ya kufanyika uchunguzi mwili wa mwanamke wa kwanza alitambulika Kwa Jina la Alesi Yaledi Ndondo mwenye umri wa miaka 35 waligundua kuwa kifo Cha mwanamke huyo kilikuwa Cha kawaida(hakuuawa).
Aidha Kamanda Malya amesema pia walikuta mwili wa mwanamke mwingine anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 ambaye jina halifahamika na mwili wake umefikishwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma