Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu amesema kuwa Serikali inapaswa kuchukua hatua kulinusuru zao la pamba ambalo bei yake inashuka kwa kasi kila mwaka.
Ado amesema kuwa amesikitishwa sana kuona zao la pamba ambalo awali lilijulikana kama “dhahabu nyeupe” limetelekezwa na Serikali. “Nimejulishwa kuwa mwaka huu, Pamba inauzwa kwa Wastani wa Tsh. 1000. Hata viwanda vya kuchambua pamba vingi vimekufa na hakuna mkakati wa serikali wa kuvifufua. Kwa ujumla Serikali imemtelekeza Mkulima wa Pamba”- alisisitiza Ado.
Akizungumza na wananchi wa Kata Banemhi katika Jimbo la Bariadi, Ado amesema kuwa Serikali inapaswa kuongeza ruzuku au kuanzisha utaratibu wa fao la bei ili kupandisha bei ya zao la Pamba.