Serikali kwa kushirikiana na madaktari bingwa pamoja na wadau wa afya mkoani Shinyanga wameendesha kampeni ya utoaji huduma ya matibabu ya afya bila malipo ijulikanayo kama Afya Code, leo ikiwa ni siku ya pili ya utoaji wa matibabu hayo yanayotarajia kufanyika kwa muda wa siku nne katika uwanja wa CCM Kambarage uliopo manispaa ya Shinyanga.
Akizungumuza mara baada ya kutembelea kwenye mabanda ya utoaji huduma mbalimbali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameeleza namna ambavyo serikali serikali ya awamu ya sita inavyoendelea kuboresha huduma za afya ndani ya mkoa huo ambao zaidi shilingi Bilioni 30 zimetokewa kwaajili ya vifaa tiba, ujenzi wa miundombinu na madawa.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amebainisha huduma zitakazotolewa na wataalam wa magonjwa mbalimbali ndani ya eneo hilo lakini pia kuwasihi wananchi kujitokeza kupata matibabu kama vile saratani ya kizazi, saratani ya matiti pamoja na tezi dume kwa wanaume.
Nao wadau wa sekta ya afya mkoani humo wameeleza manufaa ya kuanzishwa kwa cliniki hiyo ambapo aitasaidia kufanya tathimini ya uhitaji na magonjwa yaliyokithiri ndani ya mkoa huo.
Zoezi hilo la upimaji wa afya bila malipo ndani ya mkoa wa Shinyanga linatarajia kufikia tamati ifikapo Julai 27, 2024.