Beki aliyesajiliwa na kutambulishwa na Simba akitokea Coastal Union, Lameck Lawi ameanza rasmi mazoezi Ubelgiji, baada ya kufanya vipimo katika klabu ya K.A.A Gent inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Akizungumza kwa njia ya simu, kutoka Ubelgiji; “Naendelea vizuri na tayari nimeanza kufanya mazoezi na timu hii nafikiri suala la mimi kuuzwa au kufanya majaribio wenye nafasi nzuri ya kuzungumza ni viongozi,”
Amesema Lawi na kuongeza “Mimi nafanya kazi yangu iliyonileta mara baada ya hatua ya kwanza ya kufanya vipimo kukamilika sehemu ya pili ni mazoezi ambayo sasa ndio naendelea nayo”