Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru 2024 amezindua Daraja la kinyambi linalounganisha kata za Nyamisangura na Nkende ambalo linagharimu kiasi cha shilingi Milion 549 ikiwa nifedha za tozo ya mafuta.
Akizindua Daraja hilo kiongozi wa mbio za Mwenge Uhuru kitaifa Godfrey Mnzava amezitaka Taasisi zote za Serikali kuhakikisha zinatumia mfumo wa NEst katika shughuli za maendeleo.
“Hii unaondoa urasimu katika Ile kuona tunapeana kazi hapana Mkandarasi anaomba kazi anapewa kulingana na uwezo badala ya kutegemea matangazo kwenye mbao tumetoka huko nahili Tarura Wilaya Tarime niwapongeze mmtekeleza ipasavyo”Alisema Godfrey Mnzava kiongozi mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024.
Kwa upande wake meneja wa Tarura Wilaya ya Tarime Charles Marwa amesema kipindi cha Nyuma eneo hilo lilikuwa changamoto kubwa nandipo serikali ikaanza kuchukua hatua ya matengenzo kupita fedha za tozo za mafuta kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 549.
” Tulipita tukaona namna wananchi walivyokuwa wakipata changamoto yakupita katika eneo hili nasi tukasema haiwezekan tukawasilisha Serikali nakazi ikaanza mara Mmoja na sasa Mradi umefikia asilimia 85 ya utekelezaji wake”Alisema Mhandis Charles Marwa Meneja wa Tarura Wilaya ya Tarime.
Baadhi ya wananchi Wakizungumza Kwa Nyakati Tofaut wameishukuru Serikali kwanamna ambavyo imetekeleza Mradi kwani walikuwa wanapoteza ndugu zao kutokana nakuzunguka umbali mrefu.