Serikali ya DR Congo , imetangaza kusitisha shughuli zote zisizohusiana na michezo katika jiji la Kinshasa , baada ya mwishoni mwa juma lililopita, watu 9 kupoteza maisha baada ya kukanyagana wakati wa tamasha la mwanamuziki lililoongozwa na mwimbaji wa nyimbo za Injili Mike Kalambayi.
Naibu waziri mkuu anayehusika na mambo ya ndani, Jacquemin Shabani, amesema matamasha yaliyopangwa kufanywa kwenye viwanja vya Stade de Martyrs na Stade de Tata Raphael yamezuiwa kwa muda likiwemo lile la mwanamuziki Fally Ipupa.
Tags: MICHEZO