Treni ya reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) iliyokuwa ikielekea Dodoma kutokea Dar es salaam siku ya tarehe 30 Julai 2024, katika Stesheni ya Kilosa na Kidete ilisimama kwa muda wa masaa mawili kufuatia hitialafu ya umeme iliyoripotiwa kusababisha na wanyama na ndege (Bundi na Ngedere)
Mafundi walisema kuwa tatizo hilo limetokana na kukatika kwa umeme kulikosababishwa na wanyama na ndege hao kugusa nyaya zilizotandazwa juu ya reli, hivyo kusabisha mgusano wa nyaya na kisha kukatika kwa umeme katika kituo cha kupozea umeme namba 7 kilichopo Godegode majira ya saa 4:20 usiku.
Aidha mafundi walijitahidi kurekebisha tatizo hilo na saa mbili baadaye treni iliendelea na safari kisha kuwasili Domdoma majira ya saa 7:57 usiku, ambapo kufuatia tatizo hilo Shirika la Reli Tanzania limeomba radhi kwa watumiaji wa huduma hiyo.
#KonceptTvUpdates