Timu za Chelsea na Napoli zinataka kubadilishana wachezaji Romelu Lukaku ajiunge na Napoli, huku Victor Osimhen akienda Chelsea FC.
Lukaku amekubali kupunguzwa mshahara wake ili kuhamia Napoli ambao msimu ujao watakuwa chini ya kocha kipenzi cha Lukaku Antonio Conte.
Chelsea wanajadili mpango wa Lukaku kujiunga na Napoli, huku Osimhen akitarajiwa kuhamia klabu hiyo kwa mkopo.