Polisi wa Merseyside wameeleza zaidi kuhusu tukio la kusikitisha lililotokea mapema wiki hii ambapo kijana wa miaka 17 alishtakiwa kwa mauaji ya wasichana watatu katika hafla ya kucheza densi. Hafla hiyo, iliyofanyika mjini Southport na kujulikana kama “Taylor Swift”, iliisha kwa maafa baada ya wasichana hao kushambuliwa kwa kisu.
Majina ya watoto waliouawa ni Bebe King mwenye umri wa miaka 6, Elsie Dot Stancombe mwenye umri wa miaka 7, na Alice Dasilva Aguiar mwenye umri wa miaka 9. Tukio hili lilitokea siku ya Jumatatu katika mji wa Merseyside, na limeacha jamii ikiwa katika majonzi na mshangao mkubwa.
Kijana huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani baadaye Alhamisi, akikabiliwa na mashtaka ya mauaji pamoja na makosa 10 ya kujaribu kuua. Aidha, watoto wanane na watu wazima wawili walijeruhiwa katika shambulio hilo, ambapo baadhi yao wameripotiwa kuwa bado katika hali mbaya.
Kwa mujibu wa polisi, mshitakiwa ambaye jina lake halijawekwa wazi kwa sababu ya umri wake, pia anakabiliwa na shtaka la kumiliki kifaa butu. Polisi wa Merseyside walitoa taarifa hizo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliowekwa usiku wa manane, wakieleza juhudi zao za kuhakikisha haki inatendeka na usalama unarejeshwa katika jamii.
#KonceptTvUpdates