Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewahimiza waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuiombea nchi dua na viongozi wake waendelee kudumisha amani, mshikamano utulivu kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.
Dkt.Mwinyi aliyasema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa Msikiti wa Rahman Taveta, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 2 Agosti 2024.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema hakuna maendeleo pasipokuwepo amani na utulivu.
#KonceptTvUpdates