Klabu ya Simba imekamilisha tamasha lake la Simba Day 2024 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya APR FC ya Rwanda.
Mabao ya Simba katika mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa yamefungwa na Debora Fernandez dakika ya 47′ na jingine limefungwa na Edwin Balua dakika ya 67′ huku Steven Mukwala akipoteza mkwaju wa penati dakika ya 44′.
Mechi inayofata Simba atavaana na mtani wake wa jadi, Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii, Agosti 08, 2024 katika uwanja huo huo wa Kwa Mkapa.