Waziri wa Fedha Tanzania, Mwigulu Nchemba katika ukurasa wake wa X ameipongeza Simba SC kwa kuwa waasisi wa tamnasha la kufungua msim mpya maarufu kama Simba Day.
“HAPPY SIMBA DAY Mnajua mimi sio mwanasimba; Lakini buana, 1) Simba wameasisi hii mambo ya Matamasha ya Vilabu- hili ni jambo zuri. 2) Wameset viwango vya mechi na mafanikio Kimataifa na Mimi ni Shabiki wa SIMBA ya Kimataifa. 3) Simba haipati tabu kujaza uwanja iwe tamasha au mechi ya kimataifa. USIMCHUKIE MTU KWA KUFANIKIWA. SIMBA NGUVU MOYA!!!!!”, aliandika.
Kilele cha Simba Day mwaka 2024 inafanyika leo katiaka uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo katika tamasha hilo Simba SC itacheza na timu kutoka Uganda APR FC.
#KonceptTvUpdates