Imeandikwa na Jemedari Saidi
Ni mimi ndo macho yangu ya Kimakonde MABOVU au ndiyo ukweli? Sijamuona msemaji wa vilabu Afrika kwenye shughuli nzima ya GONGOWAZI leo, nini kimemkuta Ally Kamwe? Wapi amefichwa na kwanini?
Afisa habari wa klabu wapi ataonekana kama sio kwenye shughuli nyeti ya klabu? Zembwela na Kitenge wamekodiwa na Haji ametokea ndani akiwa mfanyakazi ambaye yuko chini ya Kamwe, inakuaje mkuu wa idara hayupo shughulini?
Nimeambiwa yeye Ali Kamwe ndo alikuwa kinara wa maandalizi na hadi mpango wa kuweka BIG SCREEN pale Uhuru uliratibiwa na yeye, sawa basi hakupewa nafasi ya kushika mic, ndo hata kutambua mchango wake tu imekua shida?
Sijasikia akitajwa popote pamoja na mlolongo mreeefu wa shughuli iliyokuwa na ratiba rasmi na ile alokuja nayo KALIKONJI, hata kutamka jina la Kamwe imekuwa nongwa nayo?
Yani ametambulishwa mpaka AMISA MOBETO ila Ali Kamwe aaaah! Tulisema mwanzo kwamba viongozi wa klabu wasikwepe jukumu lao la kutamka kuhusu idara ya habari ya klabu, nani kiongozi na nani kazi yake nini, najaribu kumfikiria Ali Kamwe huko aliko anajisikiaje?
Ameshatoka kwenye OB VAN ya AzamTV alikokuwa ana angalia matukio au bado ana angalia mechi huko huko? Wacha tuendelee kupiga mtori, nyama ziko chini kabisaaaa!.