Klabu ya Yanga imekamilisha tamasha lake la Wiki ya Wananchi 2024 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kwa kuwatandika mabingwa wa Kagame Cup Red Arrows mabao 2-1 ya Zambia.
Mabao ya Yanga katika mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa yamefungwa na Mudathir Yahya dakika ya 64′ na Aziz Ki dakika ya 90’+3′ kwa mkwaju wa penati huku bao la Red Arrow likifungwa mapema katika dakika ya 6 na Ricky Banda.
Mechi inayofata ni ya watani wa Jadi Simba na Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii, Agosti 08, 2024 katika uwanja huo huo wa Benjamin Mkapa.
Huku matajiri wa Jiji Azam FC wakivaana na Coastal Union wa Tanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya pili ya Ngao ya Jamii katika Dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.