Mtu Mmoja aliyefahamika kwa jina Moja la Semeni,Mkazi wa Kijiji cha Bunduki wilayani Mvomero mkoani Morogoro amefariki dunia baada ya kuzama wakati akiogelea katika Mto Ngerengere.
Akizungumza na waandishi wa habari shuhuda wa tukio hilo Alphonsi Ernesto ameeleza Semeni alizama Jumamosi Agosti 3 mwaka huu wakati akiogelea ni ya malisho na Jioni ya Agosti 03 ambapo walifika mtoni hapo kwa ajili ya kunawa mikono ambapo Semeni alivua nguo na kuogelea licha ya kukatazwa kutoogelea alikaidi mawazo yao.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Inspekta Fadhili Makala ameeleza zoezi la uokoaji limeanza tangu jana jioni majira ya saa 11:30, zoezi ambalo halikuzaa matunda na kusitishwa baada ua kufika saa 12 jioni na kulazimika kuendelea na zoezi hilo hii leo lililodumu kwa saa Nane mwili wake ulipopatikana.