Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa bei elekezi ya zao la mpunga kuwa shilingi 900 kwa kilo moja ikiongezeka kutoka ile ya awali ambayo wakulima walikuwa wakiuza zao hilo kwa shilingi 570 kwa kilo moja Mkoani Morogoro.
Rais Dkt. Samia ametoa maelekezo hayo leo Agosti 05, 2024 akiwa Mkoani Morogoro wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ifakara ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku sita Mkoani humo.
Sambamba na hayo, Rais Dkt. Samia amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kusimamia kikamilifu bei mbalimbali za mazao kuhakikisha wakulima wanauza mazao yao kwa bei halali na yenye tija ili wakulima kupata faida katika kilimo wanacho kifanya.
Tags: HABARI