Afisa Mkaguzi wa Bodi ya Nyama Tanzania (TMB), John Joshua amewahamasisha Wananchi kula nyama yenye ubora kwa kukaguliwa na kupewa kibali cha kuuzwa kwenye maduka yanayouza nyama kote nchini.
Afisa Joshua ameyaeleza hayo leo Agosti 05, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika Viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma.
Licha ya wito huo Joshua amewaalika watanzania kutembelea katika banda la bodi hiyo kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma ili kupata elimu kuhusiana na ubora wa nyama.