Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ( TPLB ) Almas Kasongo amesema msimu ujao watatoa adhabu kwa Maofisa Habari wa timu wanaochekesha na kushindwa kuzungumzia Mpira.
“Kuna Muda unamsikiliza Ofisa Habari wa timu na kujiuliza, huyu ni kiongozi wa timu au mchekeshaji? Niseme tu ndugu zangu, msimu ujao tutadili na watu hawa kwa kuwapa adhabu “ alisema Kasongo.