Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza umuhimu wa usafi wa mazingira baada ya kutembelea kiwanda cha tumbaku cha Mkwawa Leaf na kupata tathmini ya shughuli zake.
Rais Samia alizungumza siku ya Jumanne, Agosti 6, 2024, wakati akizindua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kiwanda cha Sigara cha Mkwawa Leaf pamoja na upanuzi wa kiwanda cha uchakataji tumbaku kilichopo mkoani humo.
Katika ziara hiyo, Rais Samia alioneshwa sehemu ya kiwanda inayohusika na uchakataji tumbaku, ambapo kiwanda hiki kimepangwa kuwa na madaraja mawili ya uzalishaji: “primary” na “secondary.” Daraja la kwanza (primary) litalenga kuandaa tumbaku ili isiharibike kwa muda wa takribani miaka 10, hali inayotarajiwa kuongeza usalama wa mazao ya wakulima wa tumbaku.
Aidha, uwepo wa daraja la kwanza utaongeza uwekezaji, kwani wawekezaji kutoka Dubai na mataifa mengine wataweza kufanya uzalishaji katika kiwanda hicho, hivyo kuchangia katika kuimarisha pato la taifa. Rais Samia aliwahimiza viongozi na wadau kuhakikisha kuwa suala la usafi wa mazingira linapewa kipaumbele ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea kutokana na shughuli za kiwanda hicho.
#KonceptTvUpdates