Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania ( TPLB ) Almas Kasongo ameweka wazi kuwa ratiba ya Ligi Kuu Bara iko tayari na wataitoa hadharani ndani ya siku mbili.
Kasongo amesema ratiba hiyo imezingatia vitu vingi vya msingi vya kuujenga mpira na kila mmoja ataifurahia.
“Maboresho ya kanuni pamoja na ratiba yetu ya ligi viko tayari. Boimanda Karim ( Ofisa Habari wa Bodi ) ataviweka hadharani ndani ya siku hizi mbili.
“ Tunajua tumechelewa kuitoa ratiba, lakini kuna vitu tulikuwa tunavizingatia, hivyo naamini hii ni ratiba nzuri na kila mmoja ataifurahia “ alisema Kasongo.
Ligi hiyo ambayo bingwa wake mtetezi ni klabu ya Yanga SC inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Agosti 16.