Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ya NBC Tanzania, Almas Kasongo amesema kuwa baadhi ya kanuni za ligi msimu ujao wa 2024/25 ni kuwa uwanja ambao hautakuwa na viti elfu tatu (3,000) kwaajili ya mashabiki havitatumika kwenye michezo ya Ligi Kuu.
Kasongo ameyazungumza hayo leo, Agosti 6, 2024 kwenye semina ya waandishi wa habari liyosimamiwa na bodi hiyo ambapo amesisitiza kuwa viti 3,000 ndio itakuwa idadi ya chini kabisa ya vitu kwenye jukwaa kama eneo la kuchezea na vyumba vyavkubadilishia nguo vitakuwa vinakidhi viwango.
Aidha Kasongo ameongeza kuwa kanuni zinazitaka klabu kuwa na wachezaji wasiopungua wawili kutoka timu za vijana watakao kuwa sehemu ya mchezo katika mechi za ligi kuu.