Waandamanaji nchini Uingereza waliojifunika nyuso zao kupinga uhamiaji wameripotiwa kuharibu sehemu ya hoteli ambayo imekuwa ikitumika mama makao kwa waomba hifadhi katika mji wa Rotherham.
Machafuko yameripotiwa , huku waandamanaji wanaopinga uhamiaji wakipambana na polisi.
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amewaonya waandamanaji wa siasa kali za mrengo wa kulia kwamba watawajibishwa kwa kushiriki katika ghasia hizo mbaya zaidi nchini Uingereza katika kipindi cha miaka 13.