Waandamanaji wavamia makazi ya Waziri mkuu, maarufu ‘Ganabhaban’, mjini Dhaka, Bangladesh, kufuatia hatua ya Waziri Mkuu Sheikh Hasina kukimbia nchini baada ya maandamano ya wiki kadhaa.
Jeshi la Bangladesh lilimwezesha Waziri Mkuu Sheikh Hasina ” kuondoka salama.”
Licha ya serikali ya Bangladesh awali kujaribu mara kwa mara kusitisha maandamano hayo kwa njia mbalimbali kama kuvilaumu vyama vya upinzani, kuweka amri za kutotoka nje, na kukata huduma za mitandao ya mawasiliano hatua hizi zote hazikufanikiwa na waandamanaji walifurika maeneo mbalimbali nchini humo.