Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametembelea banda la sekta ya maji mkoa wa Morogoro na kuzungumza na watumishi wa sekta hiyo katika maonesho ya nanenane kanda ya Mashariki yanayofanyika Morogoro.
Akizungumza na watumishi hao Waziri Aweso ametoa maagizo kwa sekta hiyo kuhakikisha wanawaunganishia wananchi wanaomba kupatiwa huduma ya maji kuunganishiwa ndani ya siku saba.
Aidha Waziri Aweso amewataka watumishi wa sekta ya maji kufanya juhudi za kuzibiti upotevu wa maji ambao unaripotiwa sehemu mbalimbali na wananchi kwakuwa wizara inatumia fedha nyingi kutibu na kuyasambaza maji.