“Penye wengi hapaharibiki neno,” wahenga waliona mbali kusema hivyo. Kama ambavyo imekuwa kawaida tukisema vitu na kurejelea misemo ya wahenga, basi ni dhahiri shahiri kulikuwa na haja ya kuwepo kwa tungo zenye busara kama hizo. Misemo ya wahenga inaakisi hekima na uzoefu wa maisha ambao unasaidia kutufundisha na kutuelekeza katika maisha yetu ya kila siku. Maneno haya yamepitishwa kutoka kizazi hadi kizazi, yakilenga kutufundisha umuhimu wa umoja, ushirikiano, na busara katika maamuzi na matendo yetu.
Katika msemo huu, “Penye wengi hapaharibiki neno,” tunafundishwa kwamba kuwa na watu wengi wenye mawazo na mitazamo tofauti kunaweza kusaidia kuepuka makosa na kuboresha maamuzi. Ni ukumbusho wa thamani ya mshikamano na ushirikiano katika jamii, familia, na hata katika mazingira ya kazi. Misemo kama hii inaendelea kuwa na umuhimu mkubwa katika maisha yetu ya kisasa, ikitukumbusha umuhimu wa kuwa pamoja na kufanya kazi kwa pamoja kwa manufaa ya wote.
Hata hivyo, maisha ya mwanadamu ni ya mpito, na wahenga waliona mbali kusema “chema hakidumu.” Tumeshuhudia watu waliokuwa wema sana kwa wenzao, lakini safari yao ya maisha haikuwa ndefu kama ambavyo watu walitarajia. Inaweza kuonekana kama fumbo kwamba watu hawa huja kama bahati, ili tujifunze namna nzuri ya kuishi. Vizazi na vizazi vitaendelea kumkumbuka Muammar Gaddafi wa Libya kutokana na uongozi wake, maono yake kwa watu wake, na alama alizoziacha katika nchi yake licha ya watu wasiopenda kuona haki na ukweli vikitendeka kuwa na nia mbaya dhidi yake kiasi cha kukatisha uhai wake kwa mateso makali.
Tangu enzi za ukoloni, Afrika ilibahatika kupata watu wenye maono mazuri kwa mataifa na watu wao. Mifano ni mingi, na hatuna shaka na hilo. Tazama kuhusu Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania, Kwame Nkrumah wa Ghana, na Nelson Mandela wa Afrika Kusini. Wote hawa walikuwa na maono na dhamira ya ukombozi wa watu wao kutoka katika minyororo ya ukandamizaji na ukoloni. Walikuwa viongozi wenye uthubutu, waliojali maslahi ya wengi, na waliona mbali kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Katika miaka ya hivi karibuni, Tanzania ilipata kiongozi mwenye maono na dhamira ya ukombozi wa taifa na watu wake kutoka katika mikono ya kibepari, John Pombe Magufuli. Alifanya kila awezalo ili kuhakikisha taifa lake linajikwamua kutoka katika lindi la umaskini kifkra na kiuchumi. Aliweza kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile SGR, mwendokasi, elimu bure, Tanzania ya viwanda, na kupunguza wimbi kubwa la upigaji serikalini na katika sekta binafsi. Hadi anaumaliza mwendo, taifa lilizizima kwa bumbuwazi na simanzi kwa kumpoteza simba yule.
Leo hii, Tanzania iko chini ya Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye hayuko mbali na mawazo ya wale waliopita. Anaendelea na juhudi za kuleta maendeleo na ustawi kwa taifa. Uongozi wake unalenga kuendeleza yale mazuri yaliyoanzishwa na watangulizi wake, huku akijitahidi kuboresha zaidi.
Tumeshuhudia uzinduzi wa miradi mablimbali katika maeneo tofati yote ikija na lengo la kuifungua Tanzania na kuifanya taifa linalojiweza kiuchumi, bila kusahau kuhakikisha watu wake wanapata huduma bora za kijamii. Kimsingi “historia ya jamii hujengwa na jamii yenyewe katika kipindi chote cha maisha ya jamii hiyo”, yapo mazuri mengi ambayo yamefanywa tangu enzi na enzi lakini usishangae kama hautayakuta katika viatbu vya kihistoria, hi ni kutokana na juhudi za makusudi zilizofanya na wapotoshaji.
Umoja, ushirikiano, na maono thabiti ya viongozi wetu ni mambo yanayotufanya tuendelee mbele kama taifa. Ni muhimu kuendelea kujifunza kutoka kwa wahenga wetu na kutumia hekima zao katika maisha yetu ya kila siku. Vilevile, tunapaswa kuthamini na kuenzi mchango wa viongozi wetu ambao wameweka mbele maslahi ya wengi na kupigania haki na maendeleo kwa ajili ya wote.
#KonceptTvUpdates