Katika mkutano wa waandishi wa habari mapema lao, kocha mkuu Miguel Gamondi alionyesha matumaini makubwa kuhusu msimu ujao, akisisitiza umuhimu wa kuzingatia sasa na siku zijazo badala ya matokeo ya zamani. “Yaliyopita yamepita, sipendelei kufuatilia sana yaliyopita,” alisema Gamondi, akithibitisha mkakati wake wa kujikita kwenye maandalizi ya sasa.
Gamondi alikiri kuwa mazingira ya ushindani yamebadilika, akiongeza kwamba hata wapinzani wao wamepiga hatua. “Huu ni msimu mpya hata wapinzani wetu pia wamebadilika; kila kitu kimebadilika,” aliongeza.
Kocha huyo ana uhakika kuhusu maandalizi ya timu yake, kiakili na kimwili. “Tupo imara kiakili na kimwili, tumejianda vya kutosha,” alisema. Ingawa hajapata fursa nzuri ya kuangalia wapinzani wao kutokana na upatikanaji mdogo wa matangazo, Gamondi hakukata tamaa. “Sijapata wasaa mzuri wa kuwatazama wapinzani wangu kwani mechi zao nyingi hazikuoneshwa,” alisisitiza.
Mkakati wa kocha ni kuweka msukumo mkubwa kwenye maandalizi ya timu yake, akitenga asilimia 75 ya juhudi zake kwa ajili ya maendeleo ya ndani na asilimia 25 kwa ajili ya uchambuzi wa wapinzani. “Ninaandaa timu yangu kwa asilimia 75, huku asilimia 25 ikiwa kwa ajili ya kumchunguza mpinzani,” alieleza Gamondi.
Kwa mipango wazi na mtazamo chanya, Gamondi na timu yake wapo tayari kukabiliana na changamoto za msimu mpya kwa kujiamini na azimio.
#KonceptTvUpdates