Chapa mashuhuri ya Dolce and Gabbana imezindua Marashi (l) ya Mbwa yaliyopewa jina la Mbwa wa Mwanzilishi wa Kampuni hiyo aitwaye Fefe.
Kampuni hiyo ya Italia imesema kuwa Marashi ya Fefe yamefanyiwa vipimo husika vyote na kuthibitishwa na Mamlaka husika za Wanyama.
Hii inasadikiwa kuwa ni mara ya kwanza kwa chapa mashuhuri duniani kuanzisha bidhaa hiyo ya Mbwa inayopatikana kwa dola za Kimarekani 99.
Domenico Dolce alianzisha Kampuni hiyo kwa ushirikiano na Stefano Gabbana mwaka 1985.