Baada ya siku mbili za mazungumzo marefu huko Doha, Hamas imemteua Yahya Sinwar kama mkuu wake mpya wa jumla, akichukua nafasi ya Ismail Haniyeh aliyeuawa mjini Tehran wiki iliyopita.
Tangu 2017, Sinwar amehudumu kama kiongozi wa kikundi ndani ya ukanda wa Gaza. Sasa atakuwa kiongozi wa mrengo wake wa kisiasa.
Uongozi wa Hamas kwa kauli moja ulimchagua Sinwar kuongoza vuguvugu hilo, afisa mkuu wa Hamas aliambia BBC.
Tangazo hilo linakuja wakati ambapo hali ya wasiwasi inaongezeka katika eneo la Mashariki ya Kati, huku Iran na washirika wake wakitishia kulipiza kisasi mauaji ya Haniyeh, ambayo wanailaumu Israel. Israel haijatoa maoni.
Cc; BBC
#KonceptTvUpdates