Rais wa DR Congo , Félix Tshisekedi hapo jana, amemshutumu mtangulizi wake, Joseph Kabila, kwa kuchochea mzozo wa usalama mashariki mwa DRC kupitia Muungano wa (AFC).
Katika mahojiano na Radio Top Congo, akiwa Brussels (Ubelgiji) ambako amekaa kwa siku chache kwa sababu za matibabu, Tshisekedi amesema alijaribu kuwasogelea wapinzani wake, lakini hawataki.