Kampuni ya META imeijumuisha Tanzania katika program ya malipo kwa watengeneza maudhui mtandaoni kupitia majukwaa yake ya Instagram na Facebook.
Kampuni hiyo imetoa masharti kadhaa kwa watengeneza maudhui ili kukidhi kunufaika na programu hiyo ikiwemo kabla ya kuomba kuunganishwa kwenye programu hiyo, mtengeneza maudhui anapaswa kuwa anazingatia sera za mapato kutoka kwa washirika wa Facebook, lazima awe na umri wa miaka 18 na kuendelea na awe anaishi katika nchi iliyoruhusiwa na kutimiza masharti ya kupata matangazo ndani ya maudhui.
Masharti kunufaika na video zinazohitajika (video on demand), muandaaji anapaswa kuwa na wafuasi 5,000, dakika 60,000 zilizotizamwa katika siku 60 zilizopita na ukurasa uwe na angalau video tano.
Kuhusu masharti ya kunufaika na video mbashara, muaandaaji anapaswa kuwa na wafuasi 10,000 na jumla ya dakika 600,000 zilizotizamwa katika siku 60 zilizopita.
#KonceptTvUpdates