“Ni matokeo mabaya lakini yenye kutupa maono wapi tunaelekea kwenye ujenzi wa kikosi chetu bora msimu huu (wa 2024/25).
Tunakila sababu ya kujivunia maendeleo ya Project yetu ya muda mrefu iliyohusisha wachezaji wengi wapya wenye vipaji vikubwa na umri mdogo.
Wana Simba matokeo ya leo (kufungwa bao 1-0 na Yanga) yasiwatie unyonge kwani tupo katika njia sahihi sana na punde tutaanza kuogelea kwenye mito ya asali.
Hii ni tofauti na msimu uliopita tulichukua ngao ya jamii lakini hatukua na timu imara ndio maana tukakosa Makombe yote, Msimu huu tumekosa Ngao lakini tunayo timu imara ya kutupa heshima hapo baadae” maneno ya Ahmed Ally, Afisa Habari wa Klabu ya Simba, baada ya Simba kufungwa bao 1-0 na Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii.