Klabu ya Azam FC imefanikiwa kutinga Fainali ya Michuano ya Ngao ya Jamii kwa kuifunga Coastal Union mabao 5-2 katika mchezo wa Nusu Fainali uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
Mabao ya Azam FC katika mchezo huo yalifungwa Gibril Sillah dakika ya 13′, Feisal Salum ‘Feitoto’ dakika ya 40′, Jhenier Blanco dakika ya 45+1′, Adam Adam dakika ya 88′ na Eva Meza dakika ya 90+3′.
Huku mabao ya klabu ya Coastal Union yakifungwa na Semfuko Charles dakika ya 27′ pamoja na Abdallah Hassan dakika ya 85′.
Azam FC itacheza Fainali na Yanga SC siku ya Jumapili ya Agosti 11, 2024 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, majira ya Saa 1:00 Usiku. Wakati Coastal Union watawania mshindi wa tatu dhidi ya Simba SC katika mchezo wa mapema majira ya Saa 9:00 Alasiri katika uwanja huo huo wa Mkapa.