Nyota wa klabu ya Yanga, Stephane Aziz Ki amefunguka sababu ya kuzipiga chini ofa za vilabu vikubwa barani Afrika kama Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, CR Belouizdad ya Algeria, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Wydad Casablanca ya Morocco na kuamua kubaki Yanga.
Akiongea na jarida maarufu la michezo Afrika Kusini, FARpost, Aziz KI amesema; “Ninajua Kaizer Chiefs na klabu zingine zinanihitaji, lakini pale mtu anapokuonesha heshima wewe pia unatakiwa kurejesha heshima.
“Rais wa Yanga (Hersi Said) alikuja kuniona Berkane, nilikuwa nacheza dhidi ya RS Berkane Morocco (2021), baadaye wakaja kwa familia Yangu kuongea na mimi mbele ya familia yangu. Kwangu mimii niliona ni zaidi ya heshima. Unanitaka mimi nipigie simu, sema Aziz nina ofa hii kwa ajili yako. Wao walikuja nyumbani.
“Walikuja kutoka Dar es Salaam hadi kwa familia yangu. Kwangu mimi hiyo ni too much, ni zaidi ya heshima wengine walikuwa wananipigia simu tu. Huwezi kupata watu 10 kama hao (Hersi). Nina Appreciate sana na nina furaha na hii project na jinsi ilivyokuja.
“Yanga walinionesha project, mpaka sasa ninaiamini project, ninamuamini Rais (Hersi). Naweza kusema Hersi Said ni kama baba yangu. Ninaiona project inavyokwenda na kazi nzuri inayofanyika, kwa sasa sio muda wa kuondoka Young Africans SC,” amesema Aziz Ki.
#KonceptTvUpdates