Leo, Wakenya katika maeneo kadhaa nchini wamejitokeza kwa ajili ya “Maandamano ya Nane Nane,” yaliyoandaliwa kupinga utawala wa Rais William Ruto. Waandamanaji wanadai kuwa serikali ya Ruto imekosa kutimiza ahadi zake na wanamtaka ajiuzulu.
Huku maandamano hayo yakiendelea, Rais Ruto amewataka Wakenya kuyakataa akisema yanaweza kusababisha machafuko nchini. Aliwataka wananchi kudumisha amani na kutafuta njia nyingine za kutatua matatizo badala ya kuingia barabarani.
#KonceptTvUpdates