Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imefanya mabadiliko kadhaa kwenye kanuni za Ligi Kuu, ikiwemo kuongeza uwajibikaji na kuhakikisha afya na usalama wa wachezaji.
Kanuni za Wataalamu wa Tiba
Klabu zinatakiwa kuwa na daktari msaidizi mwenye sifa au mtaalamu wa tiba ya viungo kwa mujibu wa kanuni, kwa michezo isiyozidi sita ya Ligi Kuu. Endapo klabu itashindwa kupata daktari mkuu au mtaalamu wa tiba ya viungo ndani ya michezo hiyo sita, itatozwa faini ya shilingi milioni tano (5,000,000) kwa kila mchezo, hadi kufikia michezo sita. Klabu hiyo itaondolewa kwenye Ligi Kuu na kushushwa daraja.
Vipengele vya Kanuni
Maamuzi yote yanayofanywa kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu hayatakuwa na nafasi ya kukata rufaa. Hata hivyo, kwa makosa yanayoweza kukatiwa rufaa kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni ya 79, adhabu itaondolewa na badala yake mhusika atafikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu na Kamati ya Maadili ya TFF.
Kanuni Mpya za Ligi
1. Klabu zimepewa mamlaka ya kusimamia maandalizi ya michezo, ikiwa ni pamoja na kuuza tiketi kwa njia za kielektroniki. Tiketi zitatolewa na TFF/TPLB.
2. Kila klabu italazimika kufanya mkutano na waandishi wa habari angalau mara moja kila mwezi.
3. Kutakuwa na siku maalum ya matangazo ya timu, ikiwa ni pamoja na kutoa matokeo ya mwisho wa mchezo.
4. Timu za Ligi Kuu zitalazimika kutangaza kila mchezo wa nyumbani kwa njia mbalimbali.
Masharti kwa Makocha na Wachezaji
1. Kocha mkuu wa klabu za Ligi Kuu kutoka nje ya bara la Afrika anatakiwa kuwa na Pro Diploma, huku kocha msaidizi akiwa na Diploma.
2. Kocha wa timu ya Ligi Kuu kutoka ndani ya Tanzania lazima awe amefundisha klabu ya Ligi Kuu au timu ya Taifa kwa miaka mitatu iliyopita.
Masharti ya Usajili na Mechi za Mchujo
1. Timu itakayoshindwa kufika kituoni kwa michezo mitatu ya Ligi bila sababu za msingi itafukuzwa kushiriki Ligi hiyo.
2. Katika mechi za mchujo, timu itakayochezesha mchezaji ambaye usajili wake una kasoro itatozwa faini ya shilingi milioni moja (1,000,000) hadi milioni tano (5,000,000) na kupoteza mchezo husika.
Kombe la Muungano: Kutakuwa na shindano la Kombe la Muungano litakalohusisha timu mbili kutoka Tanzania Visiwani na mbili kutoka Tanzania Bara.
#KonceptTvUpdates