“Mwalimu Nyerere katika mojawapo ya kauli zake nyingi aliwahi kusema kwamba CCM siyo mama yangu, CCM siyo mama yangu na ikiacha misingi yake nitaiacha, ilikuwa kauli ya Mwalimu kuhusu chama alichokianzisha, kwa hiyo unataka mimi niseme kwa mazingira yoyote yale vyovyote itakavyokuwa sitahama CHADEMA? ni mama yangu? Niliingia CHADEMA miaka 20 iliyopita na nimekuwa hapa miaka yote hii na Mungu anirehemu niendelee kuwa CHADEMA wakati nayo ikiendelea kuishi, lakini CHADEMA siyo dini na siyo mama yangu, ni chama cha siasa kikiondoka kwenye misingi yake iliyonipeleka nikajiunga nacho nitaondoka, nitakuwa sina sababu ya kubaki na hiyo siyo dhambi kwa sababu hiyo siyo dini na siyo mama yangu nikitumia maneno ya Mwalimu, ni chama cha siasa, vyama vya siasa huja na kuondoka, sisi binadamu tunakuja na kuondoka” Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Tundu Lissu akizungumza katika mtandao wa kijamii wa Clubhouse hivi karibuni.
Chanzo : Jambo TV