Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapongeza Yanga sc baada ya Kuichapa Simba bao Moja kwa bila, Mechi ya Ngao ya Jamii iliyopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagrama Rais ameandika “Hongereni Yanga kwa ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii. #KariakooDerby”
“Huku Taifa likiendelea kuchapa kazi, tunatarajia burudani safi ya msimu mpya wa Ligi Kuu toka kwenu Watani wa Jadi pamoja na Azam, Coastal Union, Dodoma Jiji, Fountain Gate, JKT, KMC, Kagera Sugar, KenGold, Mashujaa, Namungo, Pamba Jiji, Singida Black Stars, Tabora United na Tanzania Prisons”