Mwanamuziki kutoka Nchini Marekani Romeo Miller ambaye alipata umaarufu mkubwa kwa kufanya kazi na baba yake mzazi mtayarishaji wa Muziki Master P, ambaye pia ni Movie Star huko Marekani amewasili Jijini Arusha usiku wa kuamkia leo kwaajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kitalii ikiwemo kushiriki kwenye Tamasha kubwa la Kitalii na kiutamaduni La Maasai Global Festival litakalo fanyika Ijumaa na jumamosi hii Viwanja vya Eden Garden Njiro Tanzania.
Kabla ya Tamasha hilo Romeo atashiriki kufanya shughuli mbalimbali za Kutangaza utalii wa Tanzania kwa kutembelea Hifadhi za Arusha National Park.