Mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga SC dhidi ya Simba umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Bao pekee la Yanga katika mchezo huo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii uliopita uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, limefungwa na Kiungo mshambuliaji, Maxi Nzingeli dakika ya 44′.
Sasa rasmi Yanga itacheza fainali dhidi ya Azam FC siku ya Jumapili ya Agosti 11, 2024 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, majira ya Saa 1:00 Usiku.
Wakati Coastal Union watawania mshindi wa tatu dhidi ya Simba SC katika mchezo wa mapema majira ya Saa 9:00 Alasiri katika uwanja huo huo wa Mkapa.