Mzee Msumi ambaye ni mojawapo ya wazee wa yanga amemtaka Ali kamwe kusitisha shughuli ambayo aliipanga siku ya leo kwa ajili ya kumchukua mke wake na Mwijaku (alice) ambaye aliwekwa bondi na mme wake,endapo simba ikifungwa atamuacha mke wake aolewe na Ali kamwe.
“Niwaombeni msamaha kwasababu hili jambo limegusa hisia za Watanzania, imenichukua nusu saa kumsihi Kijana wangu (Kamwe) kwa niaba ya Wazee wa Yanga, Ally alikuwa sahihi akachukue yule Mke (Alice) kwa matamshi ya yule Bwana Mdogo (Mwijaku) lakini tukiangalia thamani ya utu wa Mwanamke na Ubinadamu sio jambo sahihi yeye kama amemchoka yule Mwanamke ni bora angemwandikia talaka amuache tu”
“Sio ubinadamu kumuweka bondi au utumwa Binadamu mwingine haipo tena, tunayasema haya iwe fundisho kwa Mwijaku na Wazazi wake, Mimi ningekuwa Mzazi wa yule Binti ningejua hatua gani nachukua moja taratibu za kisheria, mapenzi yako na Club yako usimgeuze Mke kama chambo kuleta haya katika Jamii”
“Niwaombe Wapenzi wa mpira hasa Mashabiki wa Simba ikitokea tena hakutokuwa na msamaha, Ally ana thamani kubwa ya Club ya Yanga na Utanzania wake na hadhi yake kama Mwanaume unaposema nakupa Mke wangu maana yake unaona hana uwezo wa kummiliki jambo sio sahihi, atakayerudia hakutokuwa na msamaha”
“Mwisho nikuombe Kijana wangu (Kamwe) Mwanaume amepewa sifa mbili kuwa na busara na hekima, unayotumia hapa ni hekima ili kumrudishia thamani yule Mwanamke, sisi Wazee tumemzuia Kijana wetu na niwaombe Wanachama wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye kuchukua mwali wetu sisi tumesitisha” Mzee Msumi kwa niaba ya Wazee wa Yanga.
#KonceptTvUpdates