Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, Agosti 9, 2024, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Juma Magoma na wenzake, yaliyolenga kuundoa uongozi wa Klabu ya Yanga madarakani na kuweka kando tuzo na amri zote zilizotolewa katika hukumu iliyowapa ushindi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Franco Kiswaga, alitoa uamuzi huo wakati wa kusikiliza marejeo ya shauri la maombi namba 187/2022, yaliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga. Katika uamuzi huo, Mahakama imekubaliana na madai ya Bodi hiyo kwamba wazee hao hawakuwa na sifa za kisheria za kufungua shauri hilo.
Zaidi ya hayo, Mahakama imeamuru Magoma, Geofrey Mwaipopo, na Abeid Mohamed Abeid kulipa gharama za uendeshaji wa shauri hilo kwa Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga. Uamuzi huu unaweka mwisho kwa jaribio la kuondoa uongozi wa klabu hiyo, huku Bodi ya Wadhamini ikipata ushindi katika shauri hilo.
#KonceptTvUpdates