NDEGE ya abiria ya Kampuni ya VoePass iliyokuwa imebeba abiria 57 na wahudumu wanne imeanguka huko Sao Paulo, Brazil na kupelekea vifo vya watu wote 61 waliokwemo kwenye ndege hiyo aina ya aina ya ATR-72.
Ndege hiyo iliondoka Cascavel katika Jimbo la Parana Nchini Brazil ikielekea Sao Paulo ambapo ilipoteza mawasiliano ikiwa angani na kuanguka kwenye makazi ya Watu na kisha kulipuka.
“Kampuni inasikitika kufahamisha umma kwamba watu wote 61 waliokuwa kwenye ndege nambari 2283 wamekufa katika eneo la tukio,” Voepass imesema katika taarifa yake kwa umma ikirekebisha idadi ya vifo tofauti na ilivyoripitiwa awali kwamba waliofariki ni 62.
Mamlaka zimesema pamoja na kwamba Ndege hiyo ilianguka kwenye makazi ya Watu, hakuna yeyote aliyejeruhiwa au kufariki kati yao isipokuwa waliofariki ni wote waliokuwemo kwenye Ndege pekee.
Hili ni janga la sita kwa ubaya zaidi la anga katika historia ya anga ya Brazil na mbaya zaidi tangu ajali ya 2009 ya ndege kutoka Rio de Janeiro hadi Paris ambayo ilitumbukia katika Bahari ya Atlantiki, na kuua watu wote 228.