Wadau mbalimbali wamejitokeza katika zoezi la kujaribu njia zitakazotumika kwenye CRDB Bank Marathon 2024 zinazotarajiwa kutimua vumbi Agosti 18,2024
Zoezi hilo limefanyika mapema leo Agosti 10, katika viwanja vya The Green Oysterbay maarufu kama viwanja vya Farasi Dara es Salaam, sehemu ambayo mbio hizo zitaanzia na kutamatikia siku hiyo ya Agosti 18.
Huu ni msimu wa tano CRDB Bank Marathon unaolenga kusambaza Tabasamu, jiandikishe sasa kushiriki mbio hizo za kasi isambazayo tabasamu kwa kutembelea tovuti ya www.crdbbankmarathon.co.tz
#CRDBBankMarathon2024
#TabasamuLimevukaMipaka
#KonceptTvUpdates